Rais wa Ufaransa Francois Hollande.
Rais wa
Ufaransa ameiambia Jamhuri ya Afrika ya Kati, wanajeshi wa Ufaransa
walioko huko watafanyakazi kuiepusha nchi hiyo isigawike, na kuwapokonya
silaha wanamgambo na makundi ya wahalifu wanaowapiga vita Waislamu.
Akiwasili
mjini Bangui kutoka Nigeria, alikohudhuria sherehe ya miaka 100 ya
muungano wa nchi hiyo, Rais Hollande alikutana na rais wa mpito wa
Jamhuri ya Afrika ya kati Catherine Samba-Panza na pia kuwahutubia
wanajeshi wa Ufaransa. Hii ni ziara ya pili ya Francois Hollande tangu
mwezi Desemba mwaka jana na inakuja wakati kukiwa na ongezeko la
wanajeshi wa kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Siku ya
Jumanne bunge la Ufaransa lilipiga kura kurefusha muda wa wanajeshi wa
Ufaransa nchini humo, licha ya Wafaransa wenyewe kutounga mkono
ushirikishwaji wa wanajeshi wao katika koloni lake hilo la zamani.
Wakati
huo huo Umoja wa Mataifa umesema watu milioni moja wameikimbia nchi hiyo
tangu kuanza kwa ghasia za kimadhehebu mwaka uliopita na kwamba watu
wapatao milioni 1.3 wanahitaji msaada wa haraka wa chakula katika nchi
hiyo ya Afrika.
Miezi
minne iliopita, Ufaransa ilituma wanajeshi wake ambao kwa sasa wamefikia
takriban 2000 katika nchi hiyo ilio na idadi kubwa ya Wakristo, na
waasi wa Kiislamu wa kundi la Seleka walichukua madaraka baada ya
mapinduzi waliyofanya mwezi Machi mwaka Jana, na wamekuwa wakisukumwa
nyuma na wanamgambo wa kundi la "anti-balaka."
Kando na
kuwepo kwa wanajeshi wa Ufaransa, Wanajeshi 6000 wa kulinda amani wa
Umoja wa Afrika (MISCA) pia wapo nchini humo huku takriban wanajeshi
1000 wa Umoja wa Ulaya wakiwa bado wanatarajiwa kuwasili Jamhuri ya
Afrika ya Kati.
Samba Panza atoa wito wa kuundwa kikosi cha kulinda amani cha U.N
Hata
hivyo akizungumza mjini Geneva, baada ya miezi miwili ya kusimamia
shirika la Umoja wa Mataifa la ulinzi wa Raia mjini Bangui, Philippe
Leclerc, amesema bado nchi hiyo haina wanajeshi wa kutosha wa kulinda
amani.
Ulinzi mdogo ulililazimisha shirika hilo la Umoja wa Mataifa kuwahamisha baadhi ya raia.
Rais wa
mpito Samba-Panza mara kwa mara amekuwa akitoa wito wa kuundwa kwa
kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini mwake. Katibu Mkuu
wa Umoja huo Ban Ki-moon anatarajiwa kutoa ripoti wiki ijayo, ya
kuangalia uwezekano wa kukibadilisha kikosi cha MISCA kuwa kikosi cha
Umoja wa Mataifa. Netsanet Belay, Mkurugenzi wa utafiti na utetezi wa
shirika laAmnesty International, amelitaka baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa kuridhia hatua hiyo mara moja.
Kwa
upande mwengine madaktari wasio kuwa na mipaka (MSF) wamesema zaidi ya
wakimbizi 8000 waliwasili kusini mwa nchi jirani ya Chad tangu mwishoni
mwa mwezi wa January.
Hata
hivyo kundi la antibalaka linasemekana linawafuata Waislamu kule
wanakokwenda na kujaribu kuwashambulia wakati wakijaribu kukimbia
ghasia.
Chanzo, dw.de/swahili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro






Post a Comment
Post a Comment