Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This



Kaimu Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) mwezi Novemba, 2014 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba kipindi cha usajili kwa malipo ya ada ya kawaida (Shilingi 50,000/=kwa wanaojisajili CSEE na Shilingi 30,000/= kwa wanaojisajili QT ) kimeongezwa kutoka tarehe 28 Februari, 2014 hadi tarehe 31 Machi, 2014.

Watahiniwa watakaojisajili kuanzia tarehe 1 Aprili, 2014 hadi tarehe 30 Aprili, 2014 watatakiwa kulipa ada  ya kawaida pamoja na faini mpaka usajili utakapofungwa rasmi tarehe 30 Aprili, 2014.

Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz  .Kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani kuchukua namba rejea (reference number) zinazotolewa bure na kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au Mpesa.

Imetolewa na:
KAIMU KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top