Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mtalii kutoka nchini Ujerumani anayefahamika
kwa jina la Bi . Jeanne Traska (32 ) akiwa na
muongoza wageni Athuman Juma leo majira
ya saa mbili na nusu asubui wamekwama
katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro
kwa kamba iliyonasa na kuwafanya wasiweze
kushuka chini wala kwenda juu.
Bi. Jeanne na Athuman Juma walianza
kupanda mlima kupitia Kampuni ya Nordic
Tours tarehe 18. 3. 2014 kwa kutumia njia ya
Rongai - Kibo – Marangu safari ambayo
ingewachukua siku tano.
Hadi sasa taarifa za awali zinaonyesha kuwa
Bi. Jeanne alitakiwa kwenda kileleni Kibo lakini
katika mazingira yasiyofahamika alibadili
uamuzi na kuelekea kilele cha Mawenzi
ambacho huwa hakitumiwi na watalii
isipokuwa kwa kujaza fomu maalum
inayoonyesha kuwa mgeni amekubali kwa
hiyari yake kupanda kilele hicho.
Shirika la Hifadhi za Taifa kwa kushirikiana na
Kampuni ya Nordic Tours wanaendelea na
jitihada za uokoaji kwa kutumia askari ambao
wanaelekea eneo la tukio pamoja na helikopta
itakayosaidia zoezi la uokoaji kwa kutegemea
na hali ya hewa itakavyotulia ambapo hivi
sasa kuna mawingu mazito katika eneo la
mlima.
Umma utaendelea kufahamishwa maendeleo
ya jitihada za uokoaji kadri zitakavyopatikana .
Imetolewa na
Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania
22.03 .2014

Picha ya mlima kilimanjaro

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top