MWIGIZAJI
chipukizi wa filamu Swahiliwood Zaina Ramadhan ‘Nandi’ yupo katika
wakati mgumu na anahitaji msaada wa kupata matibabu nje ya nchi baada ya
kupata matatizo ya mgongo ambapo inasemekana kuwa kuna pingiri za
mgongo zimetengana, awali alianza matibabu yake katika Hosipitali ya
Mwananyamala.Baadae
alipata rufaa kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kujaribu
kupatiwa matibabu lakini imeshindikana na anahitaji msaada wa kwenda
kutibiwa nje ya nje na inahitajika gharama kubwa akiongea na FC mama
mzazi wa Nandi amedai kuwa gharama za matibabu hapa ni 13,000,000
.
“Nawaomba
watanzania wenzangu mnisaidie kumtibia mwanangu anateseka sana hawezi
kukaa hata akilala hawezi kujigeuza, sisi kama familia uwezo wetu ni
mdogo na mtoto anazidi kuumia, nawaomba wasamaria wema mmsaidie
mwangu,”anaongea kwa uchungu Mama yake na Nandi
Awali mama
huyo aliambiwa na Daktari kuwa inahitaji fedha kwa ajili ya vipimo tu
ambayo ilikuwa ni kiasi cha 280,000/ alafu baadae tena apewe kipimo
kingine ambacho kingelifuata baada ya wiki moja, lakini hadi sasa msanii
huyo hajapatiwa matibabu kutokana na ukosefu wa fedha.
Binti huyo
alidai kuwa wakati akihangaikia jinsi ya kupata matibabu alifika katika
ofisi za shirikisho la Filamu Tanzania na kuahidiwa kusaidiwa na
shirikisho hilo badala ya kwenda kujitangaza na kuomba msaada kwa jamii,
lakini hajapatiwa msaada wowote hadi sasa.
Nandi ameshiriki filamu kama
Kuzaa si kupata, Yatima, pia msanii huyo ameshiriki katika tamthilia ya
Jua la Kiama pamoja na filamu nyingine ambazo bado hazijatoka zikiwa
bado katika uhariri.
FC ilimtafuta Rais wa
Shirikisho Simon Mwakifwamba kwa bahati mbaya simu yake ilikuwa
haipatikani hewani, lakini tulimpompigia simu katibu wa shirikisho hilo
Mr. Bishop Hiluka alisema hana taarifa hizo atajaribu kufuatilia na
kumtafuta mhusika.
Pia katibu amesisitiza wasanii
wote kujisajili katika vyama vyao ili iwe rahisi kupata taarifa
zinazowakabili, kwani bila kuwa na mawasiliano si si rahisi kuwatambua
wanachama walio salama na wale wenye matatizo.
Kwa WASAMARIA WEMA WANAOGUSWA NA MSANII HUU UNAWEZA KUTUMA PESA KWA NAMBA 0714 896 064 Mama Nandi
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro






Post a Comment
Post a Comment