Rais
Jakaya Kikwete, akibofya kitufe kuzindua mtambo wa kuhakiki takwimu za
mawasiliano kwenye Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Dar es Salaam jana.
Dar es
Salaam. Rais Jakaya Kikwete ameiagiza Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo kuhakikisha mchakato wa Sheria ya Usalama kwenye
mitandao unakamilika na kuanza kutumika, ili kudhibiti wanaotoa siri za
nchi kwa kisingizio cha uhuru wa habari.
Hayo
aliyasema jana kwenye hafla ya uzinduzi wa mtambo maalumu wa usimamizi
na uhakiki wa Mawasiliano ya Simu, (TTMS), iliyofanyika Ofisi za Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Dar es Salaam.
Rais
Kikwete alisema hakuna nchi yoyote duniani ambayo haitunzi siri zake,
kwa kuwa jambo hilo ni muhimu kiusalama, hata kwa mataifa ambayo
yamekuwa mstari wa mbele kutetea uhuru wa vyombo vya habari.
Alisisitiza
kwa kumtolea mfano aliyekuwa Jasusi wa Marekani, Edward Snowden,
anatuhumiwa kuvujisha siri za nchi hiyo kwenye mtandao, ambaye sasa
amekimbilia mafichoni Urusi. Aliwapongeza TCRA kwa hatua hiyo, akieleza
kuwa inawezesha uchumi wa nchi kupata kichocheo cha kukua kwa kuwa sasa
kutakuwa na udhibiti wa mawasiliano hasa ya simu za nje ya nchi na
kuongeza kipato kwa taifa.
Awali
Mkurugenzi wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema kufungwa kwa mitambo
hiyo, kunakwenda pamoja na kuwapo kwa kanuni mpya za mawasiliano ya
usimamizi na uhakiki wa mawasiliano ya simu (TTMS, Regulation 2013),
ambapo imewezesha Serikali kupata senti 7 kati ya 25 zinazotozwa kwa
kila dakika na nyingine zinagawanywa kwa kampuni husika.
"TCRA
imefanikiwa kuilipa Hazina mgawo wa mwezi Oktoba, kwa mujibu wa Sheria
ya TMMS Sh1.6 bilioni, leo tutakabidhi malipo ya Sh1.6 bilioni malipo ya
Novemba hatimaye mwezi Machi tutalipa ya Desemba," alisema Nkoma.
Chanzo, mwananchi
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro






Post a Comment
Post a Comment