Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Photo: Mbaroni kwa kuuza mkono wa Albino
JESHI la Polisi mkoani Rukwa, likishirikiana na polisi mkoani Tabora pamoja na kikosi kazi maalumu cha kitaifa (TASK FORCE), limefanikiwa kuwatia nguvuni watu 9 waliokuwa wakisakwa kwa muda mrefu. Watu hao wamekuwa wakitafutwa kwa tuhuma za kumkata mkono mtoto Mwigulu Matonange (10), ambaye ni mlemavu wa ngozi na kuuuza kwa Sh milioni 600.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwarwanda, alisema watuhumiwa hao walikuwa wakisakwa kwa muda mrefu kutokana na mtandao mkubwa waliokuwa nao.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Weda Mashilimu (29), Nickon Kadogoo (25), Peter Msabato (32), Ignas Sungura (27), Faraja Mwezimpya (31) na Kurwa Hamisi (29) wote wakazi wa Kijiji cha Ilemba, mkoani Rukwa.

Kamanda huyo aliwataja watuhumiwa wengine ambao ni Hamis Mnywanywa, ambaye ni mganga wa jadi na mkazi wa Karema mkoani Katavi, James Paskali (24) mkazi wa Majimoto mkoani Katavi pamoja na Ibrahimu Tella (27), mkazi wa Kijiji cha Masanula-usule mkoani Shinyanga.

Kamanda alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao ni matokeo ya uchunguzi wa kina uliokuwa unafanywa na polisi hao kupitia mawasiliano ya simu na taarifa mbalimbali za kipelelezi.

Baada ya kuhojiwa, mtuhumiwa huyo alidai kuwa yeye na wenzake hao waliagizwa mkono huo na mganga wa jadi aitwaye Rashid Manywanywa, ambapo aliwaahidi angemlipa kila mmoja Sh milioni 600 iwapo wangempelekea mkono huo.

Alisema kuwa baada ya tukio la kumkata mtoto huyo mkono na kumpelekea mganga huyo, alidai kuwa hana fedha zote hizo, kwani wao walishindwa kutumia akili kwa kuwa hata yeye ni masikini angelipata wapi fedha zote hizo, hivyo hawezi kununua mkono huo.

endelea kusoma

http://mzizima-24.blogspot.com/2013/05/mbaroni-kwa-kuuza-mkono-wa-albino.html
IGP Said Mwema 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwarwanda alisema watuhumiwa hao walikuwa wakisakwa kwa muda mrefu kutokana na mtandao mkubwa waliokuwa nao, hatimaye baadhi wamefanikiwa kukamatwa huku wengine bado wakiendelea kutafutwa.
Sumbawanga. Polisi katika Mkoa wa Rukwa likishirikiana na Polisi wa Tabora pamoja na kikosi kazi maalumu cha kitaifa, limefanikiwa kuwatia nguvuni watu tisa waliokuwa wakisakwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za kumkata mkono, Mwigulu Matonange(10) mlemavu wa ngozi Februari 15 mwaka huu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwarwanda alisema watuhumiwa hao walikuwa wakisakwa kwa muda mrefu kutokana na mtandao mkubwa waliokuwa nao, hatimaye baadhi wamefanikiwa kukamatwa huku wengine bado wakiendelea kutafutwa.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Weda Mashilimu(29),Nickon Kadogoo(25), Peter Msabato(32),Ignas Sungura(27),Faraja Mwezimpya (31) pamoja na Kurwa Hamis (29) wote wakiwa ni wakazi wa Kijiji ha Ilemba Rukwa.
Aliwataja watuhumiwa wengine ambao ni Hamis Mnywanywa ambaye ni mganga wa jadi na mkazi wa Karema Katavi,James Paskali(24) mkazi wa majimoto, pamoja na Ibrahimu Tella(27) mkazi wa kijiji Masanula-Usule Shinyanga.
Kamanda alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kulifuatia uchunguzi wa kina uliokua unafanywa na polisi hao kupitia mawasiliano ya simu na taarifa mbalimbali za kipelelezi ambapo siku ya April 22 walifanikiwa kumnasa Nickon Kadogoo akiwa Katavi na mkono huo akiupeleka mkoani Tabora ambapo angepata soko.
Baada ya kuhojiwa mtuhumiwa huyo alidai kuwa yeye na wenzake hao waliagizwa mkono huo na mganga wa jadi aitwaye Rashid Manywanywa, ambapo aliwaahidi angemlipa kila mmoja Sh600 milioni kama wangempelekea mkono huo.
Alisema baada ya tukio la kumkata mtoto huyo mkono na kumpelekea mganga huyo alidai kuwa hana fedha zote hizo kwani wao walishindwa kutumia akili kwa kuwa hata yeye ni maskini angelipata wapi fedha zote hizo, hivyo hawezi kununua mkono huo.
Baada ya kuona soko limeshindikana ndipo walipoamua kufanya mawasiliano na watu wengine na kuhakikishiwa katika Mikoa ya Tabora na Shinyanga kuna soko la uhakika ndipo safari ya kuelekea huko ikaanza.
Kwa upande wake, mganga huyo wa jadi alikiri kuwaagiza watuhumiwa hao mkono huo na kudai kuwa alitaka kutumia kutengenezea chombo cha usafiri ambacho alidai kuwa ni ungo ambao unatumika na wachawi kusafiria nyakati za usiku.
Kamanda huyo alisema watuhumiwa wote kutoka mikoa hiyo wamekamatwa na polisi na bado upelelezi unaendelea mara baada ya kukamilika watafikishwa mahakamani wakati wowote.
Chanzo:gazeti la mwananchi

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top