Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This




MWANAUME aliyefahamika kwa jina la baba Salome, mkazi wa Tandika jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alimdhalilisha mkewe (mama Salome) baada ya kufumaniwa gesti akiwa na mwanaume mwenzake ambapo madai yalisema, walikuwa katika hatua za mwisho za kuingiliana kimwili...

Aibu hiyo ya mwaka ambayo ilionekana pia kama kituko ilijiri Mei 3, mwaka huu ndani ya gesti moja maarufu iliyopo Devi’s Corner –Tandika, jijini Dar es Salaam.

Awali ilidaiwa kuwa, mwanaume huyo na baba Salome mwenye mke na watoto wawili wanaomtegemea kwa kila kitu, walionekana wakiingia kwenye gesti moja ambayo pia ipo maeneo hayo hali iliyozua maswali kwa watu waliokuwa wakiwafahamu.


“Unajua tatizo lilianzia wapi? Baba Salome na yule mwanaume mwenzake walionekana wakiingia gesti moja kisha wakatoka, wakaingia nyingine pia wakatoka, ndipo watu wanaowafahamu wakajiuliza kulikoni wawili hao kutembelea gesti siku hiyo, wakawafuatilia,” alisema mnyetishaji mmoja.


Akaendelea: Lakini watu waliwafahamu kwa namna mbili tofauti, baba Salome ni mtulivu, mwadilifu, mwenzake watu wanasema ana ‘katabia’ ka kutaka kuwa faragha na  wanaume wenzake bila kujulikana nini anakitaka katika usiri huo.


 Madai zaidi yakawekwa wazi kwamba, baadhi ya watu walikwenda kwenye gesti walizokwenda wawili hao na kuulizia nini walikuwa wanakitaka, ndipo siri ikawekwa wazi kwamba wanatafuta chumba cha kupumzika kwa siku hiyo lakini kwa sheria za Jiji la Dar es Salaam (kama siyo za nchi nzima), wanaume wawili hawaruhusiwi kulala chumba kimoja.
 
Chanzo kikasema: Wambeya wakawaona wakiingia kwenye gesti ya tukio, wakapewa chumba. Ndipo wakakimbia nyumbani kwa baba Salome na kumtonya mkewe, mama Salome kwamba mumewe ameingia gesti.

 Kichekesho zaidi kinaangushwa kwamba, baada ya kuambiwa mumewe amezama gesti, mama Salome ambaye ndiyo kwanza alikuwa amefika kutoka  kwenye mikopo ya Finca, alitoka mbio huku akisema anakwenda kumtoa sikio la kulia Kidawa akiamini mumewe ameingia gesti na mwanamke huyo. “Watu walimwambia mumewe hakuingia gesti na Kidawa bali mwanaume mwenzake. Kwanza mama Salome aliomba asitaniwe juu ya hilo, lakini akasisitiziwa,” alisema mtoa habari huyo. 

 Akizungumza kwa jazba na waandishi wetu nje ya gesti hiyo, mama Salome alisema kwamba alipata taarifa siku nyingi mumewe ana ukaribu na mwanaume huyo ambaye mitaani watu wanasema  anajihusisha na vitendo vya ushoga.

“Nilipozipata taarifa hizi sikuziamini, nilidhani ni Kidawa ndiyo kaingia gesti na mume wangu, maana Kidawa ndiye mbaya wangu,” alisema mwanamke huyo kisha akazama ndani ya gesti akiwa na polisi ambao haikujulikana walikotokea.


Huku mumewe na mwanaume mwenzake wakiwa hawana hili wala lile kule chumbani, mlango ulisukumwa na kufunguka ambapo mwanamke huyo aliwakuta wawili hao wakiwa wameshavua baadhi ya nguo.


Wote walishtuka kuona wameingiliwa!  “Yaani roho inauma sana, sijui ni kitu gani umekosa kwangu mpaka unakuja kwa mwanaume mwenzako jamani baba Salome,” alisema huku akilia mama Salome.

Baada ya kugundua wamenaswa, mwanamke aliyekuwa na baba Salome aliangua kilio huku  akiomba kusamehewa kwa vile yeye ni mume wa mtu, lakini kilio chake hakikusikika kwa polisi ambapo waliwafunga pingu na kuwataka kuelekea katika kituo cha polisi.

 Hata hivyo, pamoja na kilio hicho mwanaume huyo aliishia kuswekwa lupango na baadaye kuhamishiwa katika Kituo cha Polisi cha Chang’ombe kwa hatua zaidi. 

Chanzo:udakuspecially

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top