Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

*Utafiti wabaini ina kiwango kikubwa cha kemikali hatari mwilini mwa binadamu

Utafiti wa wanasayansi mbalimbali duniani unaonesha kuwa kuna madhara makubwa ya utumiaji wa vinywaji aina ya soda katika mwili wa mwanadamu
AFYA za mamilioni ya Watanzania wanaotumia vinywaji vya aina ya soda ipo hatarini, baada ya kugunduliwa uwepo wa chembechembe zenye kemikali za sumu ndani ya vinywaji hivyo, MTANZANIA Jumatano linaripoti.

Utafiti uliofanywa na Muungano wa Waandishi wa Habari za Uchunguzi Tanzania (Investigative Journalists Union of Tanzania- IJUTA) pamoja na tafiti zilizofanywa na wataalamu waliobobea katika afya ya umma duniani, umebaini kuwa vinywaji baridi aina ya soda ni hatari kuliko utumiaji wa sigara inayosababisha maradhi ya kansa katika mwili wa binadamu.
Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi mbalimbali duniani, yapo madhara makubwa ya utumiaji wa vinywaji vya aina ya soda katika mwili wa binadamu. Utafiti huo unaonyesha kuwa zipo sababu nane kuu zinazokiweka kinywaji aina ya soda kwenye kundi la vinywaji vyenye sumu ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu.

IJUTA imebaini kuwa makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi aina ya soda yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake, bila kutaja madhara ya vinywaji hivyo kwa binadamu.

Kwamba matangazo hayo yanayogharimu mamilioni ya fedha ndiyo yanayokifanya kinywaji hicho kuwa maarufu zaidi duniani, licha ya kuwa na madhara makubwa katika mwili wa binadamu.

Aidha, utafiti huo unaonyesha kuwa umaarufu mwingine wa kinywaji aina ya soda ni utamu wa kupindukia ulio ndani ya soda.

Utafiti wa IJUTA unaonyesha kuwa utamu wa kupindukia iliomo ndani ya soda unawapumbaza wanywaji ili wasisikie ladha kali ya asidi iliyomo ndani ya soda.

IJUTA imegundua kuwa kiwango cha asidi kilicho ndani ya soda hakiwekwi wazi kwa walaji kwa sababu ya kuhofia kuwa wakibaini wataacha kikutumia kinywaji hicho.

Inaelezwa pia kuwa madini ya cola yaliyo ndani ya soda yana kilevi aina kafein kinachomteka mnywaji kuwa teja wa kinywaji hicho.

Tafiti za kitaalamu zimeonyesha kuwa soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi, ugonjwa wa ini na mengineyo.

Utafiti uliofanywa nchini Marekani unaonyesha kuwa soda huwekewa ‘fructose’ (sukari) nyingi kupitia mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla.

chanzo:Mtanzania

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top