“Mimi nadhani mkuu wa mkoa na chama chake kukaa na
kufikiria kuitisha mkutano wa viongozi wa dini wenye lengo la kumaliza
tofauti za dini ambazo zinajitokeza haupo sahihi kwani ni vyema tatizo
likaangaliwa lipo wapi ili kupata majibu sahihi ya tofauti
zinazojitokeza sasa,” alisema Mtikila. Mkutano huo ulitarajiwa kufungwa
jana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi.
Akizungumza Dar es Salaam jana akiwa nje ya ukumbi wa mkutano huo, alisema kwa kawaida imani ya mtu ipo ndani ya roho yake na huwezi kuiondoa kwa maneno au kufanya mikutano bali kinachotakiwa ni Serikali kujitahidi kuondoa makosa yaliyojitokeza siku za nyuma ambayo ndiyo yamezaa tofauti zinazojitokeza.
“Mimi nadhani mkuu wa mkoa na chama chake kukaa na kufikiria kuitisha mkutano wa viongozi wa dini wenye lengo la kumaliza tofauti za dini ambazo zinajitokeza haupo sahihi kwani ni vyema tatizo likaangaliwa lipo wapi ili kupata majibu sahihi ya tofauti zinazojitokeza sasa,” alisema Mtikila. Mkutano huo ulitarajiwa kufungwa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi.
Alisema katika mkutano huo hakutakuwa na suala jipya kwani kila kitu kipo wazi na kwamba tatizo linalojitokeza wakati huu ni la muda mrefu tangu mwaka 1986 ambapo aliwahi kusema masuala ambayo yatakuja kujitokeza siku za usoni ikiwamo suala la udini.
“Mimi nadhani kwamba kuna haja ya msingi kuangalia suala hili la imani za kidini kwa undani hasa kutafuta tatizo lipo wapi,lakini siyo mtu mmoja akae na na kufanya mkutano kwa lengo la kutafuta suluhu ya migogoro ya dini wakati si jambo rahuisi kiasi hicho,”alisema.
chanzo:gazeti la mwananchi
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment