BAADA ya siku za hivi karibuni kubainika kuwa baadhi ya vijana wanaolinda makaburi ya Kinondoni wamegeuza mtaji kaburi la aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, mama mzazi Flora Mtegoa amewaomba wahusika kuacha mchezo huo mara moja.
Akizungumza kwa huzuni mama Kanumba alisema alihuzunishwa sana na kitendo hicho cha kaburi la mwanaye kugeuzwa mtaji na kumtaka mtu yeyote atakayetozwa pesa aripoti polisi mara moja.
“Inaniuma sana na naiomba serikali na watu wengine wanisaidie jamani kwa sababu wanaofanya biashara hiyo ya kulipisha watu kwa ajili ya kuliona kaburi wanakosea,” alisema Mama Kanumba.
Hivi karibuni ilibainika kuwa baadhi ya vijana wanaotunza makaburi ya Kinondoni wanatoza shilingi 5,000 kwa watu wanaotoka mikoani kwa ajili ya kuliona kaburi la Kanumba na kupiga
picha.soucce:global publisher
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment