Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa
yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.
Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka
moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.
Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa Chadema
walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa Chadema
waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.
Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli
watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari,
Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.
Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi
Post a Comment
Post a Comment