Kikongwe
wa miaka 86 anayesadikika kuwa ni mganga wa kienyeji anadaiwa kumbaka
mtoto wa miaka sita. Mzee huyo Edward Mwakalebela alibainika kufanya
uyama huo katika kijiji cha Ndanga na kukamatwa na uongozi wa kijiji
hicho.
Akizungumza na NIPASHE , mama wa mtoto huyo (jina linahifadhiwa) alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi baada ya mtoto huyo kulalamika maumivu ya tumbo.
Alisema mama yake alipoamua kumpa huduma ya kwanza kwa kumkanda na maji ya moto ndipo alipoona damu zikitoka sehemu za siri.
Alisema alipomhoji mtoto huyo alimtaja babu huyo kuwa alimuingilia kimwili na kumfanyia kitendo hicho cha kinyama na kuwa mzee huyo ambaye ni jirani yao alikuwa na mazoea ya kumtuma mtoto huyo kama mjukuu wake, kumbe alikuwa anatengeneza mazingira ya kumfanyia unyama huo.
Mama huyo aliamua kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa kijiji na aliamuru waende kituo cha polisi. Alisema kituo cha polisi walipewa PF3 kwa ajili ya matibabu na polisi walikwenda kumkamata mtuhumiwa na kumtia hatiani.
‘’Tulipokuwa kwa mwenyekiti wa kijiji babu huyo alikiri kutenda kosa hilo na aliomba msamaha akidai ni shetani tu alimpitia huku akiomba mambo hayo yamalizwe kimya kimya bila kwenda polisi jambo ambalo lilikuwa gumu kwetu kulikubali na ndipo taarifa ilipo pelekwa polisi,” alisema mama.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Dickson Mwakasinga, alikiri kuwapo kwa tukio hilo na kuwa baada ya kuletewa taarifa ya uwepo wa tukio hilo alifuata taratibu zote na kumkabidhi mtuhumiwa huyo mikononi mwa polisi wilaya kwa hatua zaidi za kisheria.
Mganga aliyemtibu mtoto huyo, Tabu Mwakalundwa alikiri kumpokea mgonjwa huyo na kudai kuwa aliingiliwa na kuharibiwa vibaya.
Mwakalundwa alisema kuwa mtoto huyo ameharibiwa sehemu zake za siri kwa kulazimishwa kufanya kitendo hicho na pia aliye kuwa anafanya tendo hilo alikuwa ni mtu mkubwa kwake.
CHANZO:
NIPASHE
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment