Neema tena kwa
beki Shomari Kapombe wa Simba ambaye amekuwa wa kwanza kupata nafasi ya kufanya
majaribio na klabu ya Sunderland inayoshiriki Ligi Kuu England.
Wako
wengine wanaoweza kupata nafasi hiyo, inategemea na uamuzi wa klabu ya Simba,
mfano Mrisho Ngassa, kama atakuwa ameongeza mkataba na klabu hiyo inayotumia
rangi nyekundu na nyeupe.
Huku kukiwa
na taarifa kwamba anatakiwa kwenda kufanya majaribio nchini Uholanzi, Kapombe
amepata bahati hiyo baada ya ujumbe wa Simba ulioungwa na Mwenyekiti wake,
Ismail Aden Rage na Mlezi, Rahma Al Kharusi maarufu kama Malkia wa nyuki
kufanya mazungumzo na mmiliki wa Sunderland, Ellis Short.
Akizungumza
jana mchana kutoka Newcastle, England, Malkia wa nyuki alisema wamekubaliana
mambo kadhaa na Short ambaye ni mmoja wa mamilionea nchini England, lakini
suala la kina Kapombe kufanya majaribio ni kati ya mambo yaliyopita.
“Kama
nilivyoeleza awali, kumekuwa na mambo mengi tumejadili lakini suala hilo la
wachezaji wa Simba kuja hapa kufanya majaribio tumelipa nafasi kubwa pia.
“Tunajua
tuna vijana wengi ambao wana uwezo mkubwa, mfano tulipoenda kuangalia mechi ya
vijana kati ya Sunderland na Newcastle, nilimueleza Short kwamba wachezaji
vijana wa Simba wana uwezo mkubwa ukilinganisha na wake, akacheka sana.
“Labda
aliona kama namtania, lakini nikamuambia tuwaleke huku kwa ajili ya majaribio.
Najua wakija huku watawaweka kwenye timu za vijana hasa kama watafuzu.
“Halafu taratibu
wataanza kuwapandisha taratibu, waliniambia kupanda kunategemea na mcehzaji
mwenye. Inaweza kuwa haraka au taratibu,” alisema Malkia wa nyuki.
Alipoulizwa
kuhusiana na suala la kwenda kufanya majaribio itakuwa ni siku gani, alisema:
“Hapa
inategemea tutakavyojipanga pamoja na mipango yao wao, maana yake litakuwa ni
suala la mawasiliano na baada ya hapo wachezaji watakuja huku.
“Furaha
kwangu ni kwamba wamekubali na aliyepitisha hilo ni mmiliki wa klabu mwenyewe.”
Malkia
amezungumzia mambo mengi kuhusiana na mkutano wao na mmiliki huyo wa
Sunderland. Zaidi soka ukurasa wa 23.
SOURCE:
GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment