Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This



Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana iliahirisha kusikiliza kesi ya madai ya kashfa inayomkabili Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR- Mageuzi), David Kafulila, hadi Machi 5, 2015.
Kafulila alifunguliwa kesi hiyo na Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Pan African Power Solutions (T) Limited pamoja na mfanyabiashara Harbinder Sigh Seth, ambaye ni mwenyekiti mtendaji wa kampuni hizo.
Kesi hiyo ilitarajiwa kusikilizwa mapingamizi ya awali yaliyowasilishwa na Kafulila kupitia kwa mawakili wake kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Walinzi wa Watetezi wa Haki za Binadamu.
Hata hivyo, usikilizwaji wa mapingamizi hayo, ulikwama kutokana na Jaji Rose Temba anayesikiliza kesi hiyo kuwa na majukumu mengine.
Katika kesi hiyo namba 131 ya mwaka 2014, walalamikaji wanaiomba Mahakama imwamuru mbunge huyo awalipe fidia ya Sh310 bilioni kwa madai ya kuwatuhumu kujipatia fedha kutoka katika Akaunti ya Escrow, kwa njia zisizo halali.
Shauri hilo, liliahirishwa na Msajili wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam, Projest Kahyoza.
Katika hatua nyingine; Hatima ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda itajulikana Jumatatu wakati Mahakama hiyo itakapopanga tarehe ya kusoma hukumu hiyo.

Tarehe hiyo ilitarajiwa kupangwa jana, lakini ilishindikana kutokana na Jaji Augustine Shangwa anayesikiliza rufaa hiyo kutokuwapo.
Akiahirisha shauri hilo, John Kahyoza alisema Jaji Shangwa hakufika mahakamani kuendelea na shauri hilo kwa kuwa hajisikii vizuri.
Katika rufaa hiyo, Sheikh Ponda anayetetewa na Wakili Juma Nassoro, anapinga hatia ya adhabu aliyohukumiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akidai kuwa hapakuwa na ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani kwa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.
Source Mwananchi

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top