Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


 Hii ndio hali halisi ya ukumbi ulioharibiwa na washabiki mjini Stuttgart, nchini Ujerumani
Polisi wakimuokoa Diamond na kama si polisi Diamond sijui ingekuwaje


Stuttgart,Ujerumani,
Usiku wa Jumamosi ya Tarehe  30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri
Mwanamuziki nyota wa Bongo Flaver  Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijukuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,ujerumani,baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show,washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.

Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki  Diamond na promota wake,
Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki
ma-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa.moja wa Djs hao alipoteza Lap top yake ,mwanadada DJ  Flor alipatwa shock mstuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo  DJ Drazee naye yupo hoi hospatal. 
Polisi nchini ujerumani wanamesema tukio hili la haibu alijawahi kutokea,kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa wanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.


Magazeti ya Stuttgart mengi kuhusu Diamondo na hii ni moja wapo ya Source yetu STUTTGARTER NACHRICHTEN DE
  • Bonyeza Hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top